"Nawaza" lyrics

"Nawaza"

Nawaa...naaawaaa...naawaaa...nawaza tu
Nawaa...naaawaaa...naawaaa...nawaza tu

Nawaza pru mpaka maka Ruge amerudi tena
Je kwa huu mziki wa sasa sijui nini angesema!?
Na nimejifunza binadamu kweli hawana jema
Yani mtoto unaemtunza ndo anakuombea ukilema
Nashangaa

Nawaza Vanny na Elizabeth clip zao zikivuja
Ndoa itaimarika eti au ndo ataifoja?!
Nawaza muchana,usiku jibu halifiki
Wanaonitukana, tuna bifu au ilimradi kiki?!
Nawaza kina Kimambi bwana wangekua wagawa ridhiki
Hivi kweli ningejulikana si wangenizima nsisike
Nlowaza leo nshawaza sana kina Kiba ugomvi kipi?!
Nikagundua ni ushamba na ujana wa kugombania mashabiki

Nawaa...naaawaaa...naawaaa...nawaza tu
Nawaa...naaawaaa...naawaaa...nawaza tu
Oooh nawaza

Huenda Steven Kanumba angelikuwepo hai
Nawaza movie zetu pia tungejidai
Nawaazaa hivi kombe la dunia hatufikagi why?!
Nawaza,tatizo ni team au uongozi haufai
Mawazo mengine mtanange bora tuache yataleta ukakasi
Je angekuepo Muzee Nyange,Uncle Shamte angepata nafasi?!
Nawaza ka ngekua na Wema Sepetu hadi leo sijui ngekua nshafulia au zaidi maendeleo

Ooh nawaza siku nikifa sijui wasafi itakufa
Nawaza sijui maradhi ama ajali itanikuta
Nawaza oh Mama Dangote nani chozi atamfuta
Nawaza sijui nyimbo zangu watazikumbuka
Eeeh
Nlowaza leo nshawaza sana nnachoshindwa kuwa kipi
Nikagundua naepusha lawama maana najijua kwa kucheat

Nawaa...naaawaaa...naawaaa...nawaza tu
Nawaa...naaawaaa...naawaaa...nawaza tu


Thanks to Mc Frank for adding these lyrics.
Writer(s): Daniel A Wellington, Juliet Ayub Miriam, Yaniv Akale, Jacob Otieno Obunga
album: "First Of All" (2022)
Diamond Platnumz - First Of All album cover
You May Also Like
Meddy - "Everything" I know you like it, when I touch your body You say be my babe and I say yes Ooh, baby come closer, isi ibaye ntoya Nsigaye nkumva, nkatwarwa maa I know love when I say I, I can tell when I feel it I...
Ya Levis - "Liballa" Oouuaahh El Maya loveee Nzangay lie Mama Donne moi ta main oui libala, libala nanana Nzambe a sangisi biso libala libala nanana Donne moi ta main oui libala libala nanana Nzambe a sangisi biso...
P-Square - "Gimme Dat" Through your hands up in the air In the air, in the air Through eeh some money in the air In the air, in the air Through your hands up in the air In the air, in the air Through eeh some money in the...
Rayvanny - "Kwetu" Sifa kwa Mola wangu Maulana Kwa mengi aliofanya Hadi mi na we kukutana, kisura Sijapanga kudanganya Nasema ukweli mama Kisa nakupenda sana, kisura Umesema wanipenda Ila maisha yangu maseke Michicha...
Mafikizolo - "Love Potion" Undenza ntoni yooh Kutheni ndingalali ebusuku booh Es'thandwa sami yeah Baby I've been thinking about you You know that I love you baby Angifun' omunye I want you baby I could do anything for you...